Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Linda Akili Yako

Linda Akili Yako

Pakua:

  1. 1. Nataka kufanya mema.

    Ila nafsi yapambana—

    Je, kweli nitaweza.

    Kufanya vya kutosha.

    Ninakesha na kusali,

    Ndivyo umenifunza kufanya.

    Nikipatwa na woga,

    Yehova wanishauri

    (KORASI)

    Nilinde moyo nayo akili,

    Nikazie mambo mema.

    Sikubali kurudi nyuma.

    Nalinda moyo nitatulia.

  2. 2. Nataka kukupendeza,

    Ila mimi nalemewa,

    Maisha yanichosha

    Najihisi sifai.

    Lakini ninainuka

    Na kuhubiri habari njema.

    Nitashinda huzuni.

    Yehova wanifariji.

    (KORASI)

    Nalinda moyo nayo akili,

    Nakazia mambo mema.

    Sikubali kurudi nyuma.

    Nalinda moyo nitatulia.

    N’tatulia.

    (DARAJA)

    Sitaacha kuondoa

    Mawazo mabaya kamwe—

    Sina shaka na sisumbuki.

    Yehova Baba umeniwezesha.

    Umeniwezesha.

    (KORASI)

    Nalinda moyo nayo akili,

    Nakazia mambo mema.

    Sikubali kurudi nyuma.

    Nalinda moyo nitatulia.