Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Kwa Imani

Kwa Imani

(Zaburi 27:13)

Pakua:

  1. 1. Kwa nini niogope?

    Nimwogope adui?

    Nikiwa na Yehova,

    Sitatetemeshwa.

    Mungu wangu yupo nami.

    (KORASI)

    Kwa imani, ninalo tumaini.

    Kwa imani, siogopi kamwe.

    Nikiwa na Yehova,

    Nitasonga mbele,

    Najua Mungu yuko nami—

    Kwa imani.

  2. 2. Watumishi wa kale

    Kwa ushikamanifu.

    Walivumilia.

    Watathawabishwa.

    Watafufuka hakika.

    (KORASI)

    Kwa imani, ninalo tumaini.

    Kwa imani, siogopi kamwe.

    Nikiwa na Yehova,

    Nitasonga mbele,

    Najua Mungu yuko nami—

    Kwa imani.

    (DARAJA)

    Kwa imani, nayaweza yote.

    Kwa imani, sina shaka.

    Na kwa imani

    Ninaweza kushinda

    Navumilia mateso.

  3. 3. Nasubiri kwa hamu

    Ahadi za Mungu.

    Niwe imara.

    Hivi karibuni

    Yehova atatuokoa.

    (KORASI)

    Kwa imani, ninalo tumaini.

    Kwa imani, siogopi kamwe.

    Nikiwa na Yehova,

    Nitasonga mbele,

    Najua Mungu yuko nami—

    Kwa imani,

    Kwa imani.

(Ona pia Ebr. 11:1-40.)