Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Nitaenda kwa Nani?

Nitaenda kwa Nani?

Pakua:

  1. 1. Nimemtii Yesu

    Kwenye hali ngumu.

    Ni mwanga wangu

    Namsikiliza.

    Mchungaji mwema,

    Ananifundisha.

    Huniongoza,

    Kwenye njia bora.

    (KIBWAGIZO)

    Kwa nini nisikie

    Sauti za wapinzani,

    Wenye nia mbaya

    Wanitoe njia hi’?

    (KORASI)

    Nitaenda kwa nani?

    Nikabilipo matatizo?

    Nitaenda kwa nani?

    Kuna hatari

    Kufuata mgeni.

    Namsikiliza Yesu tu.

  2. 2. Nahisi kuridhika

    Naye hunitunza,

    Tuna upendo

    Miongoni mwetu.

    Ninatazamia

    Baraka za Mungu.

    Katuma Mwanaye

    Awe Mwokozi.

    (KIBWAGIZO)

    Sitasikiliza

    Sauti za wapinzani.

    Kwa nini nitoke

    Niache njia hii?

    (KORASI)

    Nitaenda kwa nani?

    Nikabilipo matatizo?

    Nitaenda kwa nani?

    Kuna hatari

    Kufuata mgeni.

    Namsikiliza Yesu tu.

    (KORASI)

    Nitaenda kwa nani?

    Nikabilipo matatizo?

    Nitaenda kwa nani?

    Kuna hatari

    Kufuata mgeni.

    Namsikiliza Yesu tu.

    Nitaenda kwa nani?

    Kamwe, kamwe sitapotoshwa.