Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Nyumbani

Nyumbani

Pakua:

  1. 1. Nyakati nyingine,

    Nahisi kupotea,

    Shida maishani

    Zaniweka mbali na Ufalme.

    Ila haniachi kamwe.

    Yehova alinitafuta.

    (KORASI)

    Yeye hunishika mkono.

    Huniepusha na maumivu.

    Hunirudisha kwenye zizi—nyumba yake.

    Siko peke yangu nyumbani.

  2. 2. Mahali salama.

    Wakati wa dhoruba

    Napata amani

    Na rafiki wanaoniboresha.

    Unapojihisi upweke,

    Mwombe Yehova akusikie.

    (KORASI)

    Atakutafuta urudi,

    Hakuna Baba kama Yehova.

    Atakurudisha katika familia,

    Huko peke yako.

    (DARAJA)

    Nyumbani tushangilie:

    “Na karibu nyumbani!”

    Ulipotoka;

    Twafurahi kukuona.

    Karibu.

    Nyumbani.

    (KORASI)

    Amekupata na kukubeba.

    U salama mbali na madhara.

    Kwa familia yake.

    Una wenzako hapa

    Nyumbani.