Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Ungejibuje?

Ungejibuje?

Ungejibuje?

Ni Nini Kimekosekana Katika Picha Hii?

Soma Yoshua 2:15-18; 6:15-21; 7:1, 20, 21. Kisha utazame picha. Kuna kasoro gani? Andika majibu yako kwenye mistari iliyo hapa chini.

1. ․․․․․

2. ․․․․․

3. ․․․․․

4. ․․․․․

ZUNGUMZENI PAMOJA:

Mungu ana maoni gani kuhusu kuchukua kitu ambacho si chako?

Katika Toleo Hili

Jibu maswali haya na utaje mistari ya Biblia ambayo haijaonyeshwa.

UKURASA WA 5 Danieli alijulikana kuwa na sifa gani? Danieli 6:________

UKURASA WA 6 Watu wote wanapaswa kujua nini kukuhusu? Wafilipi 4:________

UKURASA WA 28 Watu wote wanapaswa kuwa na maoni gani kuhusu ndoa? Waebrania 13:________

UKURASA WA 28 Tamaa inapotunga mimba huzaa nini? Yakobo 1:________

Watoto Watafute Picha

Je, unaweza kupata picha hizi katika toleo hili? Kwa maneno yako mwenyewe, eleza jambo linalotendeka katika kila picha.

Unajua Nini Kuhusu Manabii?

Soma 2 Mambo ya Nyakati 18:1–19:3. Kisha ujibu maswali yafuatayo.

5. ․․․․․

Taja jina la nabii aliyechukiwa na Mfalme Ahabu.

6. ․․․․․

Kwa nini Ahabu alimchukia nabii huyo?

7. ․․․․․

Nabii huyo alimwambia Ahabu nini, naye Ahabu aliitikia namna gani?

ZUNGUMZENI PAMOJA:

Huenda ukahitaji kuiga ujasiri wa nabii huyo wakati gani?

▪ Majibu kwenye ukurasa wa 14

MAJIBU YA UKURASA WA 31

1. Kuta za Yeriko zilianguka chini kabisa kabla ya Waisraeli kuvamia jiji hilo.

2. Kamba ambayo Rahabu alining’iniza ilikuwa nyekundu si bluu.

3. Akani aliiba vazi, kipande cha dhahabu, na shekeli za fedha, si sanamu.

4. Walishambulia wakati wa mchana si usiku.

5. Mikaya.

6. Alitangaza hukumu za Yehova dhidi ya Ahabu.

7. Kwamba Ahabu angekufa vitani. Ahabu aliamuru Mikaya atiwe kizuizini.