Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Samaki Anayetumia Nishati Yake Vizuri

Samaki Anayetumia Nishati Yake Vizuri

Je, Ni Kazi ya Ubuni?

Samaki Anayetumia Nishati Yake Vizuri

Ili watokeze gari lenye nguvu, lisilotumia nishati nyingi, na lisiloharibu mazingira, wanasayansi walichunguza eneo ambalo wengi hawakutarajia, chini ya bahari! Samaki anayeitwa boxfish anayepatikana kwenye matumbawe yaliyo kwenye bahari za tropiki ana muundo unaofaa kutengeneza gari jepesi, linaloenda kwa kasi na kutumia nishati kidogo.

Fikiria hili: Samaki huyo anaweza kuogelea kwa kasi akisonga umbali unaolingana na mara sita ya urefu wa mwili wake kwa sekunde. Lakini hatumii nguvu ili asonge kasi hivyo. Umbo lake humwezesha kusonga kwa kasi bila kutumia nishati nyingi. Wahandisi walitengeneza gari lenye muundo wa samaki huyo na kulijaribu kwenye barabara yenye upepo mkali iliyo chini ya ardhi na wakagundua kwamba gari hilo hukata upepo kwa njia bora zaidi kuliko magari mengine.

Samaki huyo ana ngozi ya nje yenye mifupa ambayo humfanya asonge kwa nguvu lakini bado awe mwepesi. Maji yanayozunguka kwa kasi kando ya samaki huyo humfanya asiyumbeyumbe bahari inapochafuka. Kwa hiyo, samaki huyo ana uwezo mkubwa wa kudhibiti mwili wake hata anaposonga kwa kasi na anakingwa asiumie.

Wahandisi wanaamini kwamba samaki huyo atawasaidia kutokeza gari salama, jepesi, na lisilotumia mafuta mengi. Dakt. Thomas Weber, mtafiti na mbuni anasema hivi: “Kusema kweli tulishangazwa kwamba kati ya viumbe wote, samaki huyo anayeonekana mzembe ndiye angechaguliwa kutokeza muundo wa gari linaloenda kwa kasi na kutumia nishati kidogo.”

Una maoni gani? Je, samaki huyo anayetumia nishati yake vizuri alijitokeza mwenyewe? Au alibuniwa?

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 10]

Boxfish: © Hal Beral/V&W/SeaPics.com; car: Mercedes-Benz USA