Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Ungejibuje?

Ungejibuje?

Ungejibuje?

Ni Nini Kimekosekana Katika Picha Hii?

Soma Matendo 10:9-48. Kisha utazame picha. Ni vitu gani vimekosekana? Andika majibu yako kwenye mistari iliyo hapa chini na ukamilishe picha hii kwa kuchora vitu ambavyo havipo.

1. ․․․․․

2. ․․․․․

3. ․․․․․

ZUNGUMZENI PAMOJA:

Unafikiri Yehova alikuwa akimfundisha Petro jambo gani? DOKEZO: Soma Matendo 10:28, 34, 35. Unaposhughulika na watu wa rangi au tamaduni nyingine, unaweza kuonyesha jinsi gani kwamba umejifunza kutokana na simulizi hili kumhusu Petro?

Watoto Watafute Picha

Je, unaweza kupata picha hizi katika toleo hili? Kwa maneno yako mwenyewe, eleza jambo linalotendeka katika kila picha.

Katika Toleo Hili

Jibu maswali haya na utaje mistari ya Biblia ambayo haijaonyeshwa.

UKURASA WA 9 Wanadamu hawawezi kugundua nini? Mhubiri 3:________

UKURASA WA 10 Ni nani ambao wamepewa dunia? Zaburi 115:________

UKURASA WA 13 Ili tuwe na furaha lazima tutambue nini? Mathayo 5:________

UKURASA WA 19 Mipango huvunjika wakati gani? Methali 15:________

Unajua Nini Kuhusu Mwamuzi Samsoni?

Soma Waamuzi 13:1–16:31. Sasa jibu maswali yafuatayo.

[Picha katika ukurasa wa 31]

4. ․․․․․

Alikuwa wa kabila gani?

5. ․․․․․

Aliwakomboa Waisraeli kutokana na taifa gani?

6. ․․․․․

Kweli au si kweli? Aliishi baada ya nabii Samweli.

ZUNGUMZENI PAMOJA:

Kwa nini Samsoni alikuwa na nguvu sana?

DOKEZO: Soma Waebrania 11:32-34.

Ulifurahia sehemu gani katika hadithi ya Samsoni, na kwa nini?

▪ Majibu kwenye ukurasa wa 22

MAJIBU YA UKURASA WA 31

1. Hakuna viumbe wenye miguu minne.

2. Hakuna vitu vinavyotambaa.

3. Hakuna ndege.

4. Dani.—Waamuzi 13:2-5.

5. Wafilisti.—Waamuzi 13:1.

6. Si kweli.