Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Chakula cha Wadudu Kinachopatikana kwa Urahisi

Chakula cha Wadudu Kinachopatikana kwa Urahisi

Chakula cha Wadudu Kinachopatikana kwa Urahisi

● Wadudu wanapenda kula chakula wanachopata kwa urahisi kilicho na kalori nyingi. Wanapata chakula hicho kwa urahisi kwenye maua. Kama tu mikahawa, maua huwavutia wadudu kwa rangi nyangavu zinazopendeza. Wadudu hutua juu ya maua hayo na kuanza kula chavua au kunyonya nekta.

Wadudu huwa wanyonge hasa baada ya kulala kwenye baridi. Kwa hiyo, viumbe hao wenye damu baridi wanahitaji nishati ya jua ili wapate nguvu. Maua mengi huwaandalia wadudu chakula na vilevile mahali ambapo wanaweza kuota jua. Acheni tuchunguze mfano unaojulikana sana.

Maua ya kibibi yanayoitwa oxeye yanapatikana kwa wingi katika maeneo mengi ya Ulaya na Amerika Kaskazini. Huenda ua hilo lisionekane kuwa la pekee, lakini ukilichunguza kwa makini utaona kuna utendaji mwingi unaoendelea juu ya ua hilo. Ua hilo la kibibi ni mahali panapofaa kwa wadudu kupata kiamsha-kinywa. Petali zake nyeupe hazifyonzi joto la jua, kwa hiyo mdudu anapopumzika kwenye sehemu ya katikati ya ua hilo lenye rangi ya manjano anaweza kuota jua vizuri. *

Ili kuwavutia wadudu hata zaidi, sehemu ya katikati ya ua hilo la kibibi limejaa chavua na nekta, vyakula vyenye lishe ambavyo wadudu hufurahia. Ni mahali gani pengine pazuri zaidi ambapo mdudu anaweza kufurahia kiamsha-kinywa na kuota jua?

Kwa hiyo, wadudu wengi sana huja juu ya maua hayo ya kibibi siku nzima. Unaweza kuona mbawakawa, vipepeo maridadi, nyenje, na nzi wa kila aina. Bila shaka, ukitazama kwa uangalifu unaweza kuona jinsi wanavyosaidiana kupata chakula.

Kwa hiyo, unapotembea mashambani tena, mbona usichunguze mimea na wadudu hao wenye kuvutia? Ukifanya hivyo, bila shaka uthamini wako kwa Muumba aliyebuni vitu hivyo vyote utaongezeka sana.

[Maelezo ya Chini]

^ fu. 4 Wanasayansi wamegundua kwamba sehemu ya juu ya ua ni yenye joto zaidi kuliko maeneo yanayozunguka.