Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Kutibu Ugonjwa Hatari wa Milimani

Kutibu Ugonjwa Hatari wa Milimani

Kutibu Ugonjwa Hatari wa Milimani

“Nchini Peru kuna safu ya milima mirefu sana inayoitwa Pariacaca . . . Nilipopanda sehemu ya juu ya milima hiyo, inayoitwa Ngazi, nilishikwa na woga kwa ghafula hivi kwamba nilitaka kujitupa chini. . . . Pia nilihisi kichefuchefu na kuanza kutapika sana hadi nilifikiri kuwa [nitakufa]. Kama ningeendelea kupanda juu huenda ningekufa, lakini hali hiyo iliendelea kwa saa tatu au nne mpaka tulipoteremka mlima huo na kufikia sehemu ambayo ningeweza kustahimili.”—José de Acosta, kutoka katika kitabu Natural and Moral History of the Indies.

MWISHONI mwa karne ya 16, Mjesuti José de Acosta wa Hispania, alikabili hali iliyotajwa hapo juu alipokuwa akipanda Pariacaca ambayo ni mojawapo ya Milima ya Andes ya Peru. Wakati huo, ilisemekana kwamba dalili hizo zilisababishwa na gesi zenye sumu zinazotokana na madini ya milima au uvundo wa miungu watundu. Lakini sasa tunajua kwamba Acosta alikuwa na dalili za ugonjwa hatari wa milimani (acute mountain sickness—AMS).

Mwili huonyesha dalili za AMS kwa sababu ya upungufu wa oksijeni katika sehemu za juu za milimani. Mtu anapokuwa huko shinikizo la hewa hupungua na mapafu huvuta kiasi kidogo zaidi cha oksijeni. *

Mara nyingi dalili za AMS huanza mtu anapokuwa katika maeneo yaliyo juu sana kwa muda wa saa nne hivi na huenda zikadumu kwa kati ya siku moja hadi nne. Wakati huo, kiasi kidogo cha oksijeni kilicho ndani ya damu kinachochea kutokezwa kwa chembe nyekundu za damu, ambazo zitasaidia mfumo wa kuzungusha damu uwe na oksijeni zaidi.

Hata hivyo, ikiwa mtu atapanda kwa kasi mno kabla ya mwili wake kuzoea, umajimaji utajikusanya kwenye mapafu au kwenye sehemu inayozunguka ubongo. Ikiwa hali hiyo haitashughulikiwa, huenda ikasababisha kifo.

Jinsi ya Kuzuia AMS

Wasafiri na wapanda milima wamejaribu mbinu mbalimbali za kuzuia AMS. Baadhi ya mbinu hizo ni:

● Kuepuka kupanda milima ikiwa una matatizo ya kupumua au upungufu wa damu.

● Dawa za kuondoa maji mwilini, kuzuia uvimbe, au dawa nyingine zozote ambazo hutumiwa kutibu au kuzuia dalili za AMS. Mwone daktari.

● Mbinu nzuri ya kutibu AMS ni kuteremka chini. Ikiwezekana unapoteremka, vaa nguo zenye joto, na upumzike unapofika chini.

Baadhi ya mandhari zenye kupendeza na kuvutia huwa milimani. (Zaburi 148:9, 13) Ikiwa utakuwa mwangalifu unaposafiri, utadumisha afya nzuri na pia kufurahia umaridadi wa uumbaji.

[Maelezo ya Chini]

^ fu. 4 Watu wengi wanaweza kusafiri hadi mita 1,800 juu ya usawa wa bahari bila kukabili tatizo lolote.

[Blabu katika ukurasa wa 20]

Mara nyingi dalili za AMS huanza mtu anapokuwa katika maeneo yaliyo juu kwa muda wa saa nne hivi na huenda ikadumu kwa kati ya siku moja hadi nne

[Blabu katika ukurasa wa 20]

Mbinu nzuri ya kutibu AMS ni kuteremka chini