Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Mfumo wa Kumwongoza Kasa

Mfumo wa Kumwongoza Kasa

Je, Ni Kazi ya Ubuni?

Mfumo wa Kumwongoza Kasa

● Watafiti wanasema kwamba kuhamahama kwa kasa kutoka maeneo anakolisha hadi fuo anazotagia mayai ni “moja kati ya matendo yenye kustaajabisha zaidi katika ulimwengu wa wanyama.” Kwa makumi ya miaka, mnyama huyo amewashangaza sana.

Fikiria hili: Kila baada ya miaka miwili hadi minne, kasa wa kike huja ufuoni kutaga—huenda akataga mamia ya mayai katika shimo moja—na kuyaficha chini ya mchanga. Punde baada ya kuanguliwa, watoto hao wa kasa huingia baharini. Wanaanza safari ya ajabu ambayo kwa ujumla ina urefu wa kilomita 12,900 hivi. Miaka mingi baadaye, kasa wa kike, ambao sasa wamekomaa hurudi kutaga mayai yao wenyewe—kwenye ufuo uleule ambao walianguliwa!

Kasa huongozwa na nini? “Ni kana kwamba walirithi ramani ya aina fulani ya kisumaku,” anasema mwanabiolojia Kenneth Lohmann wa Chuo Kikuu cha North Carolina nchini Marekani, aliyenukuliwa katika National Geographic News. Uchunguzi unaonyesha kwamba kasa anaweza kutambua alipo kwa kupima pembe na uvutano wa nguvu za sumaku za dunia. Uwezo huo wa ajabu huwawezesha wanyama hao wadogo na wasio na ulinzi wafunge safari yao yenye urefu wa kilomita 12,900 kuzunguka Bahari ya Atlantiki, “nao hufanya hivyo wakiwa peke yao bila kufuata kasa wengine,” anasema Lohmann.

Una maoni gani? Je, uwezo wa kasa wa kujiongoza ulijitokeza wenyewe, au ulibuniwa?

[Sanduku katika ukurasa wa 25]

MAMBO HAKIKA

● Baada ya kutaga na kufunika mayai, kasa wa kike huyaacha.

● Ili kuvunja koa lake, kasa anayeanguliwa hutumia jino fulani la pekee linaloitwa caruncle, ambalo baadaye hung’oka.

● Kasa hukaa baharini kwa asilimia 90 ya maisha yao.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 25]

© Masa Ushioda/​WaterF/​age fotostocky