Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Kuutazama Ulimwengu

Kuutazama Ulimwengu

Ulimwenguni

“Kila mwaka, karibu watoto milioni 3 hufa kabla ya kumaliza mwezi mmoja baada ya kuzaliwa, wengi hufa kutokana na matatizo yanayoweza kuzuiwa. Zaidi ya asilimia thelathini hufa siku wanayozaliwa.”—Shirika la Save the Children International.

Uingereza

Kulingana na kitengo cha Afya ya Umma nchini Uingereza, mwaka 2011 kulikuwa na uchafuzi mwingi wa hewa uliosababisha ongezeko la vifo katika maeneo 15 ya jiji la London. Jambo la kushangaza ni kwamba mafuta ya dizeli husifiwa kwa sababu hayagharimu sana na hayatokezi kaboni-dioksidi kwa wingi. Hata hivyo, asilimia 91 ya uchafuzi huo ulisababishwa na magari yanayotumia mafuta ya dizeli.

Urusi

Kulingana na takwimu za Shirika la Maoni ya Umma nchini Urusi za mwaka wa 2013, asilimia 52 ya Warusi ambao ni waumini wa kanisa la Othodoksi walisema kwamba hawajawahi kusoma Biblia, na asilimia 28 walisema kwamba hawasali kwa ukawaida.

Afrika

Kulingana na ripoti ya Benki ya Dunia, mizozo kuhusu umiliki wa mashamba hupunguza mazao ya kilimo na huchangia umaskini. Nusu ya eneo zima la dunia lifaalo kwa kilimo ambalo halitumiki, yaani, ekari milioni 500—liko Afrika, na uzalishaji wa kilimo barani humo ni robo tu ya uwezo wake kamili.

Marekani

Badala ya kutumia vitabu na madaftari, shule kadhaa pamoja na vyuo vikuu vinawapa wanafunzi kompyuta ndogo (tablet) zenye vitabu vilivyohifadhiwa kielektroniki, programu, na habari nyingine. Hata hivyo watu wamehoji kuhusu gharama za kutumia njia hiyo.