Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

UNAWEZA KUKABILIANA NA MKAZO—JINSI GANI?

Ni Mambo Gani Husababisha Mkazo?

Ni Mambo Gani Husababisha Mkazo?

“Watu wengi wanasema kwamba wanazidi kupata mkazo,” kinaripoti kituo kimoja cha afya kinachojulikana sana. “Maisha ya leo yamejaa mabadiliko mengi na matukio yasiyotazamiwa.” Baadhi ya mabadiliko na matukio yasiyotazamiwa ambayo yanasababisha mkazo, yanatia ndani:

  • talaka

  • kifo cha mtu unayempenda

  • matatizo makubwa ya afya

  • aksidenti mbaya

  • uhalifu

  • shughuli zenye kuchosha za maisha

  • majanga—ya asili au yanayosababishwa na wanadamu

  • changamoto shuleni au kazini

  • kuhofia kupoteza kazi na kudumisha kipato