Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

SEHEMU YA 1

Uumbaji mpaka Gharika

Uumbaji mpaka Gharika

Mbingu na dunia zilitoka wapi? Jua, mwezi na nyota, na vitu vingi duniani, vilitokea namna gani? Biblia inatoa jibu la kweli inaposema viliumbwa na Mungu. Basi, kitabu chetu kinaanza na hadithi za Biblia juu ya uumbaji.

Tunajifunza kwamba, watu wa roho ndio walioumbwa kwanza na Mungu, wakawa kidogo kama yeye. Hao ni malaika. Lakini dunia iliumbwa kwa ajili ya watu kama sisi. Halafu Mungu akaumba mwanamume na mwanamke walioitwa Adamu na Hawa, akawaweka katika bustani nzuri. Lakini hawakumtii Mungu, wakaipoteza haki ya kuendelea kuishi.

Jumla ya miaka kutoka kuumbwa Adamu mpaka Gharika kuu, ni 1,656. Wakati huo waliishi watu wengi wabaya. Huko mbinguni, walikuwako watu wa roho wasioonekana, Shetani na malaika zake wabaya. Hapa duniani, walikuwako Kaini (Kaina) na watu wengine wengi wabaya, na watu wakubwa mno. Lakini walikuwako pia watu wazuri duniani—Habili, Henoko na Nuhu. Tutasoma habari za watu hao wote katika Sehemu ya 1 tujue yaliyotendeka.

 

KATIKA SEHEMU HII

HADITHI YA 1

Mungu Aanza Kufanyiza Vitu

Hadithi ya uumbaji ya kitabu cha Mwanzo inaeleweka na kuwagusa moyo—hata watoto wadogo.

HADITHI YA 2

Bustani Nzuri

Kulingana na kitabu cha Mwanzo, Mungu alitengeneza bustani ya Edeni kuwa mahali pa kipekee. Mungu anataka dunia yote iwe kama tu bustani ile nzuri.

HADITHI YA 3

Mwanamume na Mwanamke wa Kwanza

Mungu alimuumba Adamu na Hawa na kuwaweka katika bustani ya Edeni. Walikuwa wenzi wa kwanza wa ndoa.

HADITHI YA 4

Sababu Walipoteza Makao Yao

Kitabu cha Biblia cha Mwanzo kinatueleza jinsi paradiso ilivyopotezwa.

HADITHI YA 5

Maisha ya Taabu Yanaanza

Nje ya bustani ya Edeni, Adamu na Hawa walipata taabu nyingi. Laiti wangemsikiliza Mungu, maisha yangekuwa ya furaha kwao na kwa watoto wao pia.

HADITHI YA 6

Mwana Mzuri na Mbaya

Hadithi ya Kaini na Abeli, iliyoandikwa katika Mwanzo, inatufundisha tunapaswa kuwa watu wa namna gani na pia mitazamo tunayopaswa kubadili kabla haijawa kuchelewa mno.

HADITHI YA 7

Mtu Hodari

Mfano wa Henoko unaonyesha kwamba unaweza kufanya yaliyo mema hata ikiwa watu wanaokuzunguka wanafanya yaliyo mabaya.

HADITHI YA 8

Watu Wakubwa Mno Duniani

Mwanzo sura ya 6 inasimulia kuhusu watu wakubwa mno ambao waliwaumiza watu. Watu hao ambao waliitwa Wanefili, walikuwa watoto wa malaika waliotoka mbinguni na wakajivika miili ya kibinadamu.

HADITHI YA 9

Nuhu Anajenga Safina

Nuhu na familia yake waliokoka Gharika kwa sababu walimsikiliza Mungu ingawa wengine hawakumsikiliza Mungu.

HADITHI YA 10

Gharika Kuu

Watu walicheka Nuhu alipowaambia ujumbe wa hukumu. Lakini hawakucheka maji ya gharika yaliposhuka kutoka mbinguni! Jifunze jinsi safina ya Nuhu ilimwokoa Nuhu, familia yake na wanyama wengi.