Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

HADITHI YA 16

Isaka Anapata Mke Mzuri

Isaka Anapata Mke Mzuri

JE! UNAJUA mwanamke aliye katika picha hii? Jina lake ni Rebeka. Na mwanamume anayekutana naye ni Isaka. Atakuwa mke wake. Ilikuwa namna gani?

Ilikuwa hivi, Ibrahimu baba ya Isaka alitaka kumtafutia mwana wake mke mzuri. Hakutaka Isaka aoe mwanamke wa Kanaani, kwa sababu watu hao waliabudu miungu ya uongo. Ibrahimu akamwambia mtumish wake: Nenda Harani, kwa ukoo wangu ukamtafutie Isaka, mwanangu, mke.’

Mara hiyo mtumishi wa Ibrahimu akachukua ngamia kumi akaanza safari ndefu. Alipofika karibu na ukoo wa Ibrahimu, alisimama penye kisima. Ilikuwa jioni, wakati wanawake wa mji wanapokuja kuteka maji katika kisima. Basi mtumishi wa Ibrahimu alimwomba Yehova hivi: Mwanamke atakayeteka maji na kunipa mimi na ngamia, na awe ndiye umechagua kuwa mke wa Isaka.’’

Upesi Rebeka akaja kuteka maji. Mtumishi huyo alipomwomba maji ya kunywa akampa. Kisha akaenda kuchota ya kutosha ngamia wenye kiu. Ilikuwa kazi ngumu maana ngamia wanakunywa maji mengi sana.

Rebeka alipomaliza, mtumishi wa Ibrahimu alimwuliza jina la baba yake. Akamwuliza hata kama angeweza kulala kwao usiku huo. Alijibu: ‘Baba yangu ni Betueli, kuna nafasi yako kukaa pamoja na sisi.’ Mtumishi wa Ibrahimu alijua Betueli ni mwana wa Nahori ndugu ya Ibrahimu. Basi alipiga magoti akamshukuru Yehova kwa kumwelekeza kwenye ukoo wa Ibrahimu.

Usiku huo mtumishi wa Ibrahimu aliwaambia Betueli na Labani ndugu ya Rebeka sababu iliyompeleka huko. Wote wawili wakakubali Rebeka aende naye akaolewe na Isaka. Rebeka alijibu nini alipoulizwa? Alikubali. Halafu kesho yake wakapanda ngamia wakisafiri sana kurudi Kanaani.

Walipofika jioni, Rebeka akamwona mwanamume akitembea shambani. Ni Isaka. Alifurahi kumwona Rebeka. Sara mama yake alikuwa amekufa miaka mitatu iliyopita, naye alikuwa bado amehuzunika. Isaka sasa akampenda sana Rebeka, akawa na furaha tena.