Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

SEHEMU YA 3

Kukombolewa Misri Mpaka Mfalme wa Kwanza wa Israeli

Kukombolewa Misri Mpaka Mfalme wa Kwanza wa Israeli

Musa aliwaongoza Waisraeli kutoka utumwa wa Misri kwenda kwenye Mlima Sinai, ambako Mungu aliwapa sheria zake. Baadaye, Musa akawatuma wanaume 12 wakapeleleze nchi ya Kanaani. Lakini 10 kati yao wakarudisha ripoti mbaya. Waliwafanya watu watake kurudi Misri. Kwa kukosa imani, Mungu aliwaadhibu Waisraeli kwa kuwafanya watange-tange jangwani muda wa miaka 40.

Mwishowe, Yoshua akachaguliwa aongoze Waisraeli kuingia nchi ya Kanaani. Ili kuwasaidia waichukue nchi hiyo Yehova alifanya miujiza mingi. Alifanya maji ya Mto Yordani yaache kutiririka, kuta za Yeriko zianguke, jua lisimame bila kwenda kwa siku nzima. Baada ya miaka sita, nchi hiyo ikachukuliwa kutoka kwa Wakanaani.

Kuanzia na Yoshua, Waisraeli walitawalwa na mahakimu (waamuzi) muda wa miaka 356. Twajifunza habari za wengi wao, kutia Baraki, Gideoni, Yeftha, Samsoni na Samweli. Pia twasoma habari za wanawake kama Rahabu, Debora, Yaeli, Ruthu, Naomi na Delila. Kwa jumla, Sehemu ya 3 inasimulia historia ya miaka 396.

 

KATIKA SEHEMU HII

HADITHI 34

Aina Mpya ya Chakula

Chakula hiki cha pekee kinatoka mbinguni.

HADITHI 35

Yehova Anatoa Sheria Zake

Ni sheria gani mbili ambazo ni kuu kuliko zile Amri Kumi?

HADITHI 36

Ndama ya Dhahabu

Kwa nini watu waliabudu mfano uliotengenezwa kwa hereni zilizoyeyushwa?

HADITHI 37

Hema ya Ibada

Sanduku la agano lilikuwa katika chumba cha ndani.

HADITHI 38

Wapelelezi 12

Wapelelezi kumi wanasema jambo moja, na wawili jambo tofauti. Waisraeli wanawaamini nani?

HADITHI 39

Fimbo ya Haruni Inamea Maua

Inawezekanaje maua yamee kwenye fimbo kwa usiku mmoja?

HADITHI 40

Musa Anaupiga Mwamba

Musa anapata matokeo mazuri, lakini alimkasirisha Yehova.

HADITHI 41

Nyoka wa Shaba

Kwa nini Mungu aliwatuma nyoka wenye sumu wawaume Waisraeli?

HADITHI 42

Punda Anasema

Punda anaona kitu ambacho Balaamu haoni.

HADITHI 43

Yoshua Anakuwa Kiongozi

Musa bado ana nguvu, hivyo kwa nini Yoshua anakuwa kiongozi?

HADITHI 44

Rahabu Anaficha Wapelelezi

Rahabu aliwasaidiaje wanaume wawili, naye wafanye nini?

HADITHI 45

Kuvuka Mto Yordani

Muujiza unatokea makuhani wanapokanyaga maji.

HADITHI 46

Kuta za Yeriko

Kamba inazuiaje ukuta usianguke?

HADITHI 47

Mwivi Katika Israeli

Je, mtu mmoja mbaya anaweza kusababisha matatizo kwa taifa zima?

HADITHI YA 48

Wagibeoni Wenye Hekima

Walimdanganya Yoshua na Waisraeli ili wawape ahadi, hata hivyo Waisraeli walitimiza ahadi yao.

HADITHI YA 49

Jua Linasimama Tu

Yehova anamfanyia Yoshua jambo ambalo hakuwahi kufanya na hajawahi kufanya tena tangu wakati huo.

HADITHI 50

Wanawake Hodari Wawili

Baraki anaongoza jeshi la Waisraeli vitani, hivyo kwa nini Yaeli anasifiwa?

HADITHI 51

Ruthu na Naomi

Ruthu anaacha kwao ili aishi na Naomi na kumtumikia Yehova.

HADITHI 52

Gideoni na Wanaume Wake 300

Mungu alichagua jeshi hili dogo kwa njia isiyo ya kawaida.

HADITHI 53

Ahadi ya Yeftha

Ahadi yake kwa Yehova iliathiri si yeye tu bali binti yake pia.

HADITHI 54

Mwanamume Mwenye Nguvu Kuliko Wote

Delila alijuaje siri ya nguvu za Samsoni?

HADITHI 55

Mvulana Mdogo Anamtumikia Mungu

Mungu anamtuma Samweli kumwambia Kuhani Mkuu Eli ujumbe mzito.