Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

HADITHI YA 50

Wanawake Hodari Wawili

Wanawake Hodari Wawili

WAISRAELI wanapopata taabu, wanamlilia Yehova. Yehova anawajibu kwa kuwapa viongozi hodari wawasaidie. Biblia inawataja viongozi hao, waamuzi. Yoshua alikuwa mwamuzi wa kwanza, na waamuzi wachache waliomfuata ni Othʹnieli, Ehudi na Shamgara. Lakini wanawake wawili wanaosaidia Israeli ni Debora na Yaeli.

Debora ni nabii-mke. Yehova anampasha habari wakati ujao, kisha anawaambia watu maneno ya Yehova. Debora ni mwamuzi pia. Anakaa chini ya mtende katika nchi ya vilima, na watu wanamwendea awasaidie magumu yao.

Wakati huu Yabini ndiye mfalme wa Kanaani. Ana magari ya vita 900. Jeshi lake lina nguvu sana hata Waisraeli wengi wamelazimika kuwa watumishi wa Yabini. Mkuu wa jeshi la Mfalme Yabini ni Sisera.

Siku moja Debora anampelekea Mwamuzi Baraki habari hii: ‘Yehova amesema hivi: “Chukua watu 10,000 kwenye Mlima Tabori. Nitamleta Sisera kwako huko. Nitakupa ushindi juu yake na jeshi lake.”’

Baraki anamwambia Debora hivi: ‘Nitakwenda ikiwa wewe pia utakwenda nami.’ Debora anaenda naye, lakini anamwambia Baraki hivi: ‘Wewe hutasifiwa kwa kushinda, kwa kuwa Yehova ataweka Sisera katika mkono wa mwanamke.’ Inakuwa hivyo.

Baraki anatelemka Mlima Tabori akutane na askari wa Sisera. Mara moja Yehova anafanyiza maji mengi, na askari adui wengi wanazama. Lakini Sisera anashuka katika gari lake huyo, anakimbia.

Baada ya muda kidogo Sisera anafika kwenye hema ya Yaeli. Anamkaribisha ndani, na kumpa maziwa. Yanamtia usingizi, upesi analala usingizi mwingi. Ndipo Yaeli anachukua msumari wa hema na kuupigilia katika kichwa cha mtu huyo mbaya. Baraki anapokuja, Yaeli anamwonyesha Sisera amekufa! Basi, unaona yanatimia maneno ya Debora.

Halafu Mfalme Yabini pia anauawa, Waisraeli wanakuwa na amani tena kwa muda.