Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

SEHEMU YA 4

Mfalme wa Kwanza wa Israeli Mpaka Utumwa Babeli

Mfalme wa Kwanza wa Israeli Mpaka Utumwa Babeli

Sauli (Saulo) akawa mfalme wa kwanza wa Israeli. Lakini Yehova alimkataa, Daudi akachaguliwa awe mfalme badala yake. Tunajifunza mambo mengi juu ya Daudi. Akiwa kijana, alipigana na jitu Goliathi. Baadaye alimkimbia Mfalme Sauli mwenye wivu. Kisha Abigaili mwenye sura nzuri akamzuia asitende upumbavu.

Halafu, tunajifunza mengi juu ya Sulemani (Solomono), mwana wa Daudi, aliyechukua mahali pa Daudi awe mfalme wa Israeli. Kila mmoja wa wafalme watatu wa kwanza wa Israeli alitawala kwa miaka 40. Baada ya Sulemani kufa, Israeli waligawanyika kuwa falme mbili, ufalme wa kaskazini na wa kusini.

Ufalme wa kaskazini wa makabila 10 uliendelea muda wa miaka 257 kabla ya kuharibiwa na Waashuru. Halafu miaka 133 baadaye, ufalme wa kusini wa makabila mbili ukaharibiwa pia. Wakati huu Waisraeli walihamishwa kupelekwa Babeli. Hivyo Sehemu ya 4 inazungumza historia ya miaka 510, muda ambao mambo mengi ya kusisimua yanatukia mbele yetu.

 

KATIKA SEHEMU HII

HADITHI 56

Sauli​—Mfalme wa Kwanza wa Israeli

Mungu alimchagua na kisha akamkataa, tunaweza kujifunza somo muhimu kutoka kwa Sauli.

HADITHI 57

Mungu Anamchagua Daudi

Mungu aliona nini katika Daudi ambacho Samweli hakuona?

HADITHI 58

Daudi na Goliathi

Daudi alimpiga Sauli, si kwa kombeo lake tu bali kwa silaha yenye nguvu zaidi.

HADITHI 59

Sababu Yampasa Daudi Akimbie

Sauli alimpenda Daudi mwanzoni, lakini baadaye alimwonea wivu akataka kumuua. Kwa nini?

HADITHI 60

Abigaili na Daudi

Abigaili asema kwamba mume wake ni mpumbavu, hata hivyo hilo linaokoa uhai wa mume wake kwa muda mfupi.

HADITHI 61

Daudi Anafanywa Mfalme

Daudi anathibitisha kwamba anastahili kuwa mfalme wa Israeli kwa yale anayofanya na anayokataa kufanya.

HADITHI 62

Matata Katika Nyumba ya Daudi

Kwa kosa moja, Daudi anajiletea yeye na familia yake matatizo kwa miaka mingi.

HADITHI YA 63

Sulemani Mfalme Mwenye Akili

Je kweli angemkata mtoto vipande viwili?

HADITHI YA 64

Sulemani Anajenga Hekalu

Licha ya kuwa na hekima nyingi, Sulemani alishawishiwa kufanya jambo la kipumbavu na lenye kosa.

HADITHI YA 65

Ufalme Unagawanywa

Mara tu Yeroboamu alipoanza kutawala, aliwaongoza watu kuvunja amri za Mungu.

HADITHI YA 66

Yezebeli - Malkia Mbaya Sana

Angetumia njia yoyote ile ili apate anachotaka.

HADITHI YA 67

Yehoshafati Anamtumaini Yehova

Kwa nini jeshi lingeenda kwenye pambano likiwa na waimbaji wasio na silaha wakiongoza njia?

HADITHI YA 68

Wavulana Wawili Wanaokuwa Hai Tena

Je mtu aliyekufa anaweza kuwa hai tena? Imewahi kutokea!

HADITHI YA 69

Msichana Anamsaidia Mwanamume Mwenye Nguvu

Alikuwa na ujasiri wa kusema, na matokeo yake yalikuwa ni muujiza.

HADITHI YA 70

Yona na Samaki Mkubwa

Yona alijifunza somo muhimu kuhusu kutii maagizo ya Yehova.

HADITHI YA 71

Mungu Anatoa Ahadi ya Paradiso

Paradiso ya kwanza ilikuwa ndogo; paradiso hii itaijaza dunia yote.

HADITHI YA 72

Mungu Anamsaidia Mfalme Hezekia

Katika usiku mmoja, malaika aua wanajeshi 185,000 wa Ashuru.

HADITHI YA 73

Mfalme Mzuri wa Mwisho wa Israeli

Akiwa tineja, Yosia alitenda kijasiri.

HADITHI YA 74

Mwanamume Asiyeogopa

Yeremia alifikiri alikuwa mdogo sana kuwa nabii, lakini Mungu alijua kwamba angeweza kuwa nabii.

HADITHI YA 75

Wavulana Wanne Babeli

Walifanikiwa licha ya kuwa mbali na familia zao.

HADITHI YA 76

Yerusalemu Unaharibiwa

Kwa nini Mungu aliwaruhusu maadui wa Israeli, Wababeli, waharibu Yerusalemu?