Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

HADITHI YA 73

Mfalme Mzuri wa Mwisho wa Israeli

Mfalme Mzuri wa Mwisho wa Israeli

YOSIA ana miaka minane tu anapokuwa mfalme wa makabila mawili ya kusini ya Israeli. Huo ni umri mchanga sana kwa mtu kuwa mfalme. Kwanza wazee wanamsaidia kutawala taifa.

Yosia akiisha kuwa mfalme kwa miaka saba, anaanza kumtafuta Yehova. Anafuata mfano wa wafalme wazuri kama Daudi, Yehoshafati na Hezekia. Halafu, akiwa bado kijana tu, Yosia anafanya jambo la uhodari.

Waisraeli wamekuwa wabaya sana kwa muda mrefu. Wanaabudu miungu ya uongo. Wanaabudu sanamu. Basi Yosia anatoka pamoja na watu wake na kuanza kuondoa ibada ya uongo katika nchi. Hiyo ni kazi kubwa kwa sababu watu wengi wanaabudu miungu ya uongo. Unaweza kumwona Yosia hapa na watu wake wakizivunja sanamu.

Kisha, Yosia anaweka wanaume watatu wasimamie kazi ya kutengeneza hekalu la Yehova. Fedha zinakusanywa kwa watu na wanaume hao wanaofanya kazi wanalipwa mshahara. Wanapotengeneza hekalu, Hilkia kuhani mkuu anaona humo kitu cha maana sana. Ni kitabu cha sheria ambacho Yehova alimwagiza Musa aandike zamani sana. Kilikuwa kimepotea kwa miaka mingi.

Kitabu hicho chapelekwa kwa Yosia, naye anaomba asomewe. Anaposikiliza, Yosia anaona kwamba watu hawakuwa wakishika sheria ya Yehova. Anasikitika sana na kupasua mavazi yake, kama unavyoona hapa. Anasema: ‘Yehova ametukasirikia sisi, kwa sababu baba zetu hawakuzishika sheria za kitabu hiki.’

Yosia anamwamuru Hilkia kuhani mkuu achunguze jambo ambalo Yehova atawafanyia. Hilkia anamwendea mwanamke Hul’da, nabii-mke, na kumwuliza. Anampa ujumbe huu wa Yehova ampelekee Yosia: ‘Yerusalemu na watu wote wataadhibiwa kwa sababu wameabudu miungu ya uongo na nchi imejaa ubaya. Lakini wewe, Yosia, umefanya mema, adhabu hii itatokea baada ya kufa kwako.‘