Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

HADITHI YA 98

Juu ya Mlima wa Mizeituni

Juu ya Mlima wa Mizeituni

HUYU ni Yesu juu ya Mlima wa Mizeituni. Wanaume wanne walio pamoja naye ni mitume wake. Ni ndugu Andrea na Petro, pia ndugu Yakobo na Yohana. Unaloona mbali kule ni hekalu la Mungu katika Yerusalemu.

Zimepita siku mbili tangu Yesu alipopanda mwana-punda kuingia Yerusalemu. Ni Jumanne. Mwanzoni mwa siku hiyo Yesu alikuwa hekaluni. Makuhani walitaka kumkamata Yesu wamwue huko. Lakini waliogopa kufanya hivyo kwa sababu watu wanampenda Yesu.

‘Ninyi nyoka na wana wa nyoka!’ Yesu akawaita hivyo viongozi hao wa dini. Ndipo Yesu anasema kwamba Mungu angewaadhibu kwa mabaya yote waliyofanya. Baada ya hayo Yesu anapanda Mlima wa Mizeituni, ndipo mitume hao wanne wanaanza kumwuliza maulizo. Unajua wanavyomwuliza Yesu?

Mitume hawa wanauliza mambo ya wakati ujao. Wanajua Yesu atamaliza ubaya wote duniani. Lakini wanataka wajue wakati hilo litakapotokea. Yesu atakuja tena atawale wakati gani?

Yesu anajua wafuasi wake duniani hawataweza kumwona anapokuja tena. Ni kwa vile atakuwa mbinguni, hawawezi kumwona huko. Basi Yesu anawaambia mitume wake mambo fulani yatakayokuwa yakitokea duniani anapotawala mbinguni. Ni mambo gani hayo?

Yesu anasema kutakuwako vita vikuu, watu wengi watakuwa wagonjwa na kuona njaa, uvunjaji wa sheria utakuwa mbaya sana, tena kutakuwako matetemeko makubwa ya ardhi. Pia Yesu anasema kwamba habari njema za ufalme wa Mungu zitahubiriwa kila mahali duniani. Je! tumeona hayo yakitokea leo? Ndiyo! Basi twaweza kuwa na hakika kwamba sasa Yesu anatawala mbinguni. Karibuni atamaliza ubaya wote duniani.