Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

HADITHI YA 102

Yesu Yuko Hai

Yesu Yuko Hai

UNAMJUA mwanamke huyu na wanaume wawili? Mwanamke huyu ni Mariamu Magʹda·lene, rafiki ya Yesu. Wanaume wenye mavazi meupe ni malaika. Chumba hiki kidogo ambacho Mariamu anachungulia ni mahali alipozikwa Yesu baada ya kufa. Kinaitwa kaburi. Lakini sasa mwili haupo!

Baada ya Yesu kufa, makuhani wanamwambia Pilato hivi: ‘Yesu alipokuwa hai alisema atafufuliwa baada ya siku tatu. Basi amuru kaburi lilindwe. Wanafunzi wake hawataweza kuiba mwili wake waseme amefufuliwa!’ Pilato anawaambia makuhani hao wapeleke askari wakalinde kaburi.

Lakini mapema sana siku ya tatu tangu Yesu afe malaika wa Yehova anafika mara moja. Anaondoa jiwe katika kaburi. Askari wanaogopa sana hata wanashindwa kutembea. Mwishowe, wanapochungulia kaburi, kumbe mwili hamna! Askari wengine wanaingia mjini na kuwaambia makuhani. Unajua wanalofanya makuhani hao wabaya? Wanawapa fedha askari waseme uongo. ‘Semeni wanafunzi wake walikuja usiku, tulipokuwa tumelala, wakaiba mwili huo,’ makuhani wanaambia askari hivyo.

Wakati huu, wanawake fulani rafiki za Yesu wanatembelea kaburi. Wanashangaa kukuta kaburi tupu! Mara moja malaika wawili wanatokea wakiwa na mavazi yenye kung’aa. ‘Kwa nini mnamtafuta Yesu huku?’ wanauliza. ‘Amefufuliwa. Nendeni upesi mkawaambie wanafunzi wake.’ Wanawake wanakimbia sana kama nini! Lakini njiani mwanamume mmoja anawasimamisha. Unajua ni nani? Ni Yesu!

Wanawake hao wanapowaambia wanafunzi Yesu yuko hai na wamemwona, wanafunzi hawasadiki. Petro na Yohana wanaenda mbio kwenye kaburi wakajionee, lakini ni kaburi tupu! Petro na Yohana wanapoondoka, Mariamu Magʹda·lene abaki nyuma.

Unajua mwili wa Yesu ulivyofanywa? Mungu alifanya usiwepo. Mungu hakumfufua Yesu akae katika mwili wenye nyama aliokufa nao. Alimpa Yesu mwili mpya wa roho, kama malaika mbinguni. Lakini ili aonyeshe wanafunzi wake kwamba yuko hai, Yesu anajivika mwili ambao watu wanaweza kuona.