Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Watu wa Jinsia Tofauti

Watu wa Jinsia Tofauti

SEHEMU YA 1

Watu wa Jinsia Tofauti

Unaona mvulana na msichana shuleni wakiwa wameshikana mikono huku wakitembea. Unahisi jinsi gani?

Sihisi chochote

□ Ninawaonea wivu kidogo

□ Ninawaonea wivu sana

Umeenda na marafiki kuona sinema kisha unagundua kwamba kila mtu, isipokuwa wewe, ana rafiki wa jinsia tofauti! Unahisi jinsi gani?

□ Sijali

□ Ninahisi upweke kidogo

□ Ninawaonea wivu sana

Rafiki yako mkubwa ameanza kupendezwa na mtu wa jinsia tofauti na sasa wameanzisha urafiki wa kimapenzi. Unahisi jinsi gani?

□ Ninafurahi

□ Ninawaonea wivu kidogo

□ Ninachukizwa

Mvulana na msichana, msichana na mvulana. Kila mahali unapotazama—shuleni, barabarani, madukani—kila mtu ana wake. Kila mara unapowaona, unatamani sana kuwa na wako. Lakini, je, uko tayari kuanzisha urafiki wa kimapenzi? Ikiwa uko tayari, unaweza kufanya nini ili umpate mtu ambaye atakufaa? Na ukimpata, mnaweza kufanya nini ili mbaki mkiwa safi kiadili mnapoendeleza urafiki wenu? Maswali hayo yatajibiwa katika Sura ya 1-5.

[Picha ya ukurasa mzima katika ukurasa wa 12, 13