SEHEMU YA 1
Matukio Yanayoongoza Kwenye Huduma ya Yesu
“Huyo atakuwa mkuu.” —Luka 1:32
KATIKA SEHEMU HII
SURA YA 1
Wapokea Ujumbe Kutoka kwa Mungu
Malaika Gabrieli alileta ujumbe ambao ilikuwa vigumu kuuamini.
SURA YA 2
Yesu Aheshimiwa Kabla Hajazaliwa
Elisabeti na mtoto wake ambaye hakuwa amezaliwa walimheshimu Yesu jinsi gani?
SURA YA 3
Yule Atakayetayarisha Njia Azaliwa
Mara tu baada ya Zekaria kupata tena kimuujiza uwezo wake wa kuongea, alitoa unabii muhimu.
SURA YA 4
Maria—Ana Mimba Lakini Hajaolewa
Je, Yosefu anamwamini Maria anaposema kwamba ana mimba, si kutokana na mwanamume, bali kupitia roho takatifu?
SURA YA 6
Mtoto Aliyeahidiwa
Yosefu na Maria wanapomleta Yesu hekaluni akiwa mchanga, Waisraeli wawili wenye umri mkubwa wanatabiri kuhusu maisha ya Yesu ya baadaye.
SURA YA 7
Wanajimu Wamtembelea Yesu
Kwa nini mwanzoni nyota ambayo waliona Mashariki haikuwaongoza kwa Yesu bali kwa Mfalme muuaji Herode?
SURA YA 8
Wanaokoka Kutoka kwa Mtawala Mwovu
Mambo matatu yaliyotabiriwa katika Biblia kumhusu Masihi yanatimizwa mwanzoni mwa maisha ya Yesu.
SURA YA 10
Familia ya Yesu Yasafiri Kwenda Yerusalemu
Yosefu na Maria wanachanganyikiwa wanapokosa kumpata Yesu, naye anashangaa kwamba hawakutambua mara moja mahali ambapo wangempata
SURA YA 11
Yohana Mbatizaji Atayarisha Njia
Baadhi ya Mafarisayo na Masadukayo wanapomjia Yohana, anawashutumu. Kwa nini?