Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

WIMBO NA. 6

Mbingu Zatangaza Utukufu Wa Mungu

Mbingu Zatangaza Utukufu Wa Mungu

(Zaburi 19)

  1. 1. Mbingu, nyota, zamtukuza Mungu.

    Uumbaji wake,

    angani twaona.

    Kila siku, wamsifu Mungu.

    Fahari na nguvu zake,

    mwezi watangaza.

  2. 2. Sheria ya Yehova ni kamili.

    Vikumbusho vyake,

    huongoza wote.

    Maamuzi yake yanafaa.

    Neno lake ni hakika,

    sheria ni safi.

  3. 3. Kumwogopa Yehova kwastahili.

    Nazo amri zake,

    zapita dhahabu.

    Maagizo yake hutulinda.

    Jina lake takatifu

    tunalitukuza.