Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

WIMBO NA. 12

Mungu Mkuu, Yehova

Mungu Mkuu, Yehova

(Kutoka 34:6, 7)

  1. 1. Mungu mkuu, unastahili,

    Kusifiwa zaidi,

    U Mungu mwenye haki.

    U Mweza-yote, Mwenye upendo;

    U Mungu wa milele.

  2. 2. Baba twaona, rehema zako.

    Tu watu wa mavumbi;

    Nawe waturehemu.

    Watufadhili, watuongoza,

    Daima maishani.

  3. 3. Mbingu, dunia, zakupa sifa;

    Twakusifu kwa nyimbo,

    Twakukweza milele.

    Mungu mkuu, unastahili.

    Pokea sifa zetu.