Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

WIMBO NA. 24

Njooni Kwenye Mlima wa Yehova

Njooni Kwenye Mlima wa Yehova

(Isaya 2:2-4)

  1. 1. Tazama uone,

    Mlima wa Yehova.

    Uko, juu zaidi,

    Kuliko mingine.

    Toka pande zote,

    Watu wamiminika.

    Nao waita wengi,

    Wamwabudu Mungu.

    Mdogo, mnyonge,

    Atakuwa taifa kubwa.

    Twapiga hatua,

    Yehova anatubariki.

    Umati mkubwa,

    Unajiunga nasi.

    Nao waukubali

    Ufalme wa Mungu.

  2. 2. Agizo tunalo,

    La kuhubiri Neno.

    Nasi tunatangazia

    wote Ufalme.

    Kristo atawala,

    Awahimiza wote.

    Kote duniani

    Wamsikie Yeye.

    Neno la Yehova,

    Linawafungulia njia.

    Tunayo furaha,

    Kuwasaidia wengine!

    Sote tushiriki

    Kwa kuwasaidia

    Watu wajue Mungu

    Wapate uzima.