Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

WIMBO NA. 34

Kutembea kwa Utimilifu

Kutembea kwa Utimilifu

(Zaburi 26)

  1. 1. Nihukumu, Nakutumaini;

    Na utimilifu wangu uchunguze.

    Nichunguze na unijaribu;

    Nisafishe moyo, na unibariki.

    (KORASI)

    Ee Yehova, Nimeazimia

    Kuwa mwaminifu, siku zangu zote.

  2. 2. Sikuketi na wadanganyifu.

    Nimelichukia kundi la waovu.

    Tafadhali usiniharibu,

    Pamoja na watu wapendao rushwa.

    (KORASI)

    Ee Yehova, Nimeazimia

    Kuwa mwaminifu, siku zangu zote.

  3. 3. Nyumba yako naipenda sana.

    Na ibada yako, naitanguliza.

    Nizunguke madhabahu yako,

    Nitangaze kote kazi zako zote.

    (KORASI)

    Ee Yehova, Nimeazimia

    Kuwa mwaminifu, siku zangu zote.

(Ona pia Zab. 25:2.)