WIMBO NA. 37
Kumtumikia Yehova kwa Nafsi Yote
-
1. Ee Yehova, Baba yangu,
Ninakupenda wewe sana.
Najiweka wakfu kwako;
Nitakutii sikuzote.
Ninafanya mapenzi yako.
Vikumbusho navipenda.
(KORASI)
Ee Yehova, wastahili,
Utumishi wa nafsi yote.
-
2. Kazi zako zakukweza,
Ukuu wako zatangaza.
Nami pia nikusifu;
Nilitangaze Jina Lako.
Ninakupa maisha yangu;
Nitakuwa mwaminifu.
(KORASI)
Ee Yehova, wastahili,
Utumishi wa nafsi yote.
(Ona pia Kum. 6:15; Zab. 40:8; 113:1-3; Mhu. 5:4; Yoh. 4:34.)