WIMBO NA. 40

Sisi Ni wa Nani?

Sisi Ni wa Nani?

(Waroma 14:8)

  1. 1. Wewe ni wa nani?

    Unamtii nani?

    Yule unayemwinamia,

    Huyo ndiye Mungu wako.

    Miungu wawili,

    Huwezi kuabudu.

    Hatimaye uamuzi wako,

    Wategemea moyo.

  2. 2. Wewe ni wa nani?

    Utamtii nani?

    Yupo wa kweli, yupo mwongo.

    Basi amua mwenyewe.

    Je, ni Kaisari

    Utakayemtii?

    Ama Yehova Mungu wa kweli

    Na kumtumikia?

  3. 3. Mimi ni wa nani?

    Yehova nitatii.

    Nitamtumikia Yeye,

    Niweke nadhiri zangu.

    Alininunua,

    Nishikamane naye.

    Nitayafanya mapenzi yake;

    Nitamsifu Yeye.