Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

WIMBO NA. 51

Tumejiweka Wakfu kwa Mungu!

Tumejiweka Wakfu kwa Mungu!

(Mathayo 16:24)

  1. 1. Yehova ametuvuta kwake Kristo

    Tupate kuwa wanafunzi.

    Toka juu mbinguni,

    Nuru Yake yang’aa.

    Tumekuza imani;

    Twajikana wenyewe.

    (KORASI)

    Twajiweka wakfu kwake; kwa kupenda.

    Mbele zake tunashangilia.

  2. 2. Twasimama mbele zake Mungu wetu.

    Tumtumikie milele.

    Ni shangwe kubwa sana,

    Kumtangaza kote,

    Jina lake kubeba,

    Na Ufalme kutangaza.

    (KORASI)

    Twajiweka wakfu kwake; kwa kupenda.

    Mbele zake tunashangilia.