Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

WIMBO NA. 59

Msifu Yah Pamoja Nami

Msifu Yah Pamoja Nami

(Zaburi 146:2)

  1. 1. Tusifu Yah;

    Tumwimbie!

    Uhai na vyote anatupa.

    Kila siku,

    Tumsifu.

    Ana upendo na nguvu nyingi.

    Tumwimbie na kumtukuza.

  2. 2. Tusifu Yah,

    Hutujali.

    Husikiliza maombi yetu.

    Huinua

    Wadhaifu;

    Roho yake huwaimarisha.

    Jina lake na tulitangaze.

  3. 3. Tusifu Yah.

    Mungu wetu;

    Hutufariji kukiwa shida.

    Husamehe;

    Na kuponya.

    Baraka anatumiminia.

    Njooni tumsifu kwa shangwe!