WIMBO NA. 77
Nuru Katika Ulimwengu Wenye Giza
-
1. Twaishi, siku za giza,
Nuru twaiona.
Ni kama mapambazuko,
Punde asubuhi.
(KORASI)
Mwangaza gizani;
Ujumbe wa Ufalme.
Tumaini zuri—
Giza latoweka,
Nuru yaonekana—
Mwanzo mpya.
-
2. Walio usingizini,
Muda wayoyoma.
Tuwape habari njema,
Wapate uzima.
(KORASI)
Mwangaza gizani;
Ujumbe wa Ufalme.
Tumaini zuri—
Giza latoweka,
Nuru yaonekana—
Mwanzo mpya.
(Ona pia Yoh. 3:19; 8:12; Rom. 13:11, 12; 1 Pet. 2:9.)