WIMBO NA. 96 Kitabu cha Mungu Ni Hazina Chagua Rekodi ya Sauti Kitabu cha Mungu Ni Hazina Samahani, programu ya kupakia faili hiyo imeshindwa kupakia. Pakua Video Hii Onyesha Kama Maandishi Ficha Aina ya Maandishi (Methali 2:1) 1. Kuna kitabu ambacho huwapa, Watu amani na tumaini. Mawazo yake yana nguvu nyingi; Kinafumbua macho ya watu. Ni Biblia takatifu ya Mungu. Iliandikwa kale na watu. Waliompenda sana Yehova, Walichochewa na roho yake. 2. Waliandika kuhusu ’umbaji, Ulimwengu ulivyotokea. Ukamilifu wa mtu mwanzoni. Paradiso ilivyopotea. Pia kuhusu malaika mwovu, Aliyeipinga enzi kuu. Kukawa dhambi, kifo, na huzuni, Ushindi wa Yah waja upesi. 3. Leo twaishi pindi ya pekee. Ufalme wa Mungu watawala. Twatangaza habari za Ufalme, Na baraka zitakazokuja. Biblia inazo habari njema; Ni karamu tele ya kiroho. Huwapa watu wote tumaini; Hiyo ni hazina kwelikweli. (Ona pia 2 Tim. 3:16; 2 Pet. 1:21.) Inayotangulia Inayofuata Chapa Shiriki Shiriki Kitabu cha Mungu Ni Hazina ‘MWIMBIENI YEHOVA KWA SHANGWE’ Kitabu cha Mungu Ni Hazina (Wimbo Na. 96) Lugha ya Alama ya Tanzania Kitabu cha Mungu Ni Hazina (Wimbo Na. 96) https://cms-imgp.jw-cdn.org/img/p/1102016896/sign/wpub/1102016896_sign_sqr_xl.jpg sjj 96