Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

WIMBO NA. 100

Wakaribisheni

Wakaribisheni

(Matendo 17:7)

  1. 1. Yehova huonyesha ukarimu.

    Ubaguzi hana, si mdhalimu

    Jua nayo mvua,

    hanyimi yeyote.

    Hutoa chakula kwa wote.

    Tuwafadhilipo watu wa chini,

    Twamwiga Yehova, Anathamini.

    Naye Baba yetu,

    atatufadhili,

    Kwa wema wetu na fadhili.

  2. 2. Hatuwezi kujua matokeo,

    Ya kutokuwa na upendeleo.

    Hata iwe kwamba,

    hatuwafahamu,

    Twawakaribisha kwa hamu.

    Nasi twawaambia, ‘karibuni! ’

    Wajistareheshe bila huzuni.

    Mungu awajua

    wote wamwigao.

    Wawafadhilio wenzao.