Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

WIMBO NA. 120

Igeni Upole wa Kristo

Igeni Upole wa Kristo

(Mathayo 11:28-30)

  1. 1. Bwana Yesu hakuwa na kiburi;

    Hakujitakia makuu kamwe.

    Alikuwa na jukumu muhimu;

    Lakini kajishusha sikuzote.

  2. 2. Nyote mlio na mahangaiko,

    Ichukueni nira yake Kristo.

    Mtapata burudisho la nafsi;

    Bwana wetu ana tabia-pole.

  3. 3. ‘Nyote ni ndugu,’ kasema Bwanetu.

    Msiwe mkitafuta makuu.

    Wapole wana thamani kwa Mungu;

    Watairithi dunia milele.