Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

WIMBO NA. 125

“Wenye Furaha Ni Walio na Rehema! ”

“Wenye Furaha Ni Walio na Rehema! ”

(Mathayo 5:7)

  1. 1. Mungu ni mwenye rehema!

    Hurehemu kwa kupenda.

    Hupendezwa na fadhili.

    Huturuzuku daima,

    Tunapotubu twajua,

    Husikia dua zetu.

    Anajua tu dhaifu,

    Naye anaturehemu.

  2. 2. Na tunapohuzunika,

    Tumkoseapo Mungu.

    Kristo alitufundisha

    Tusali kwake Yehova:

    ‘Tusamehe dhambi zetu,

    Tusamehevyo wengine.’

    Mambo yatakuwa sawa,

    Nasi tuwe na amani.

  3. 3. Tunaporehemu watu

    Tuonyeshe ukarimu.

    Hatutafuti pongezi,

    Bali kwa moyo mweupe.

    Mungu aonaye vyote,

    Huona rehema zetu.

    Waonyeshao rehema,

    Wanampendeza Mungu.

(Ona pia Mt. 6:​2-4, 12-14.)