WIMBO NA. 136
Malipo Kamili Kutoka kwa Yehova
-
1. Yehova ni mwaminifu, ajua,
Kuna nyakati ambazo,
Watumishi wake hupata shida,
Ilitabiriwa kale.
Ikiwa umeacha familia,
Makao au rafiki,
Utapata ndugu na dada sasa
Na uzima wa milele.
(KORASI)
Yehova na akuthawabishe.
Malipo kamili na akupe.
Kimbilio upate kwake.
Yehova kwa kweli; ni mwaminifu.
-
2. Nyakati nyingine tunalemewa,
Au kuvunjika moyo.
Nyakati nyingine yaonekana
Kuwa hatuna uwezo.
Mungu wa faraja yote Yehova,
Husikia sala zetu.
Tujapolemewa, Yehova Mungu,
Hutuimarisha sana.
(KORASI)
Yehova na akuthawabishe.
Malipo kamili na akupe.
Kimbilio upate kwake.
Yehova kwa kweli; ni mwaminifu.
(Ona pia Amu. 11:38-40; Isa. 41:10.)