Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

WIMBO NA. 141

Muujiza wa Uhai

Muujiza wa Uhai

(Zaburi 36:9)

  1. 1. Kila kitoto, tone la mvua,

    Kila mwale wa jua, kila bua​—⁠

    Vyote vyatoka, kwake Yehova.

    Miujiza ya Mungu ya kila siku.

    (KORASI)

    Basi tutumie uhai wetu

    Kumpenda Yule atupaye uhai.

    Hata tufanyeje, haununuliki.

    Bali ni zawadi​—⁠Na ni muujiza.

  2. 2. Wengine kama mke wa Yobu,

    Husema: ‘Mlaani Mungu ufe.’

    Lakini sisi, twamsifu Yah;

    Twashukuru kwa zawadi ya uhai.

    (KORASI)

    Basi tutumie uhai wetu

    Kupenda na kuwajali jirani zetu.

    Hata tufanyeje, haununuliki.

    Bali ni zawadi​—⁠Na ni muujiza.