Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

SOMO LA 5

Kusoma kwa Usahihi

Kusoma kwa Usahihi

1 Timotheo 4:13

MUHTASARI: Soma kwa sauti kile hasa kilichoandikwa kwenye ukurasa.

JINSI YA KUFANYA HIVYO:

  • Tayarisha vizuri. Elewa kusudi la kuandikwa kwa simulizi hilo. Jizoeze kusoma mafungu ya maneno, si neno mojamoja. Epuka kuongeza, kurukaruka, au kubadilisha maneno. Zingatia alama za vituo.

  • Tamka kila neno kwa usahihi. Ikiwa hujui jinsi neno linavyotamkwa, liangalie katika kamusi, sikiliza rekodi ya chapisho lililosomwa, au uombe msaada kutoka kwa msomaji mzuri.

  • Zungumza waziwazi. Tamka maneno waziwazi, inua kichwa chako na ufumbue kabisa kinywa unapoongea. Jitahidi kutamka kila silabi.