NYONGEZA A
Kweli Tunazopenda Kufundisha
Yesu alisema watu wenye mioyo minyoofu watatambua kweli wanapoisikia. (Yoh. 10:4, 27) Kwa hiyo, kila tunapozungumza na watu tunahitaji kuwaeleza kweli rahisi zinazopatikana katika Biblia. Jaribu kuanza kwa kuuliza hivi: “Je, unajua kwamba . . . ?” au “Umewahi kusikia kwamba . . . ?” Kisha tumia Biblia kufafanua kweli hiyo. Kweli rahisi ya Biblia inaweza kupanda mbegu katika moyo wa mtu, na Mungu anaweza kuikuza mbegu hiyo!—1 Kor. 3:6, 7.
WAKATI UJAO
-
1. Matukio tunayoona na jinsi watu wanavyojiendesha, ni ishara ya kwamba hivi karibuni hali zitabadilika.—Mt. 24:3, 7, 8; Luka 21:10, 11; 2 Tim. 3:1-5.
-
2. Dunia haitaharibiwa kamwe.—Zab. 104:5; Mhu. 1:4.
-
3. Mazingira yatakuwa bora na dunia itakuwa paradiso.—Isa. 35:1, 2; Ufu. 11:18.
-
4. Kila mtu atakuwa na afya kamilifu.—Isa. 33:24; 35:5, 6.
-
5. Unaweza kuishi milele duniani.—Zab. 37:29; Mt. 5:5.
FAMILIA
-
6. Mume anapaswa “kumpenda mke wake kama anavyojipenda mwenyewe.”—Efe. 5:33; Kol. 3:19.
-
7. Mke anapaswa kumheshimu sana mume wake.—Efe. 5:33; Kol. 3:18.
-
8. Mume na mke wanapaswa kuwa waaminifu.—Mal. 2:16; Mt. 19:4-6, 9; Ebr. 13:4.
-
9. Watoto wanaowaheshimu na kuwatii wazazi wao watafanikiwa.—Met. 1:8, 9; Efe. 6:1-3.
NASA, ESA and the Hubble Heritage Team (STScI/AURA)-ESA/Hubble Collaboration. Licensed under CC BY 4.0. Source.
MUNGU
-
10. Mungu ana jina.—Zab. 83:18; Yer. 10:10.
-
11. Mungu anawasiliana nasi.—2 Tim. 3:16, 17; 2 Pet. 1:20, 21.
-
12. Mungu hana ubaguzi na anatenda kwa haki.—Kum. 10:17; Mdo. 10:34, 35.
-
13. Mungu anataka kutusaidia.—Zab. 46:1; 145:18, 19.
SALA
-
14. Mungu anataka tusali kwake.—Zab. 62:8; 65:2; 1 Pet. 5:7.
-
15. Biblia inatufundisha jinsi ya kusali.—Mt. 6:7-13; Luka 11:1-4.
-
16. Tunapaswa kusali mara nyingi.—Mt. 7:7, 8; 1 The. 5:17.
YESU
-
17. Yesu ni mwalimu mkuu na sikuzote ushauri wake unafaa.—Mt. 6:14, 15, 34; 7:12.
-
18. Yesu alitabiri matukio tunayoona leo.—Mt. 24:3, 7, 8, 14; Luka 21:10, 11.
-
19. Yesu ni Mwana wa Mungu. —Mt. 16:16; Yoh. 3:16; 1 Yoh. 4:15.
-
20. Yesu si Mungu Mweza Yote.—Yoh. 14:28; 1 Kor. 11:3.
Based on NASA/Visible Earth imagery
UFALME WA MUNGU
-
21. Ufalme wa Mungu ni serikali halisi iliyo mbinguni.—Dan. 2:44; 7:13, 14; Mt. 6:9, 10; Ufu. 11:15.
-
22. Ufalme wa Mungu utaondoa serikali za wanadamu.—Zab. 2:7-9; Dan. 2:44.
-
23. Ufalme wa Mungu ndio suluhisho pekee la matatizo ya wanadamu.—Zab. 37:10, 11; 46:9; Isa. 65:21-23.
KUTESEKA
-
24. Mungu hasababishi mateso tunayokabili.—Kum. 32:4; Yak. 1:13.
-
25. Shetani anautawala ulimwengu huu.—Luka 4:5, 6; 1 Yoh. 5:19.
-
26. Mungu anaona unapoteseka na anataka kukusaidia.—Zab. 34:17-19; Isa. 41:10, 13.
-
27. Hivi karibuni Mungu atakomesha mateso.—Isa. 65:17; Ufu. 21:3, 4.
KIFO
-
28. Wafu hawajui jambo lolote wala hawateseki.—Mhu. 9:5; Yoh. 11:11-14.
-
29. Wafu hawawezi kutusaidia au kutuumiza.—Zab. 146:4; Mhu. 9:6, 10.
-
30. Wapendwa wetu waliokufa watafufuliwa.—Ayu. 14:13-15; Yoh. 5:28, 29; Mdo. 24:15.
-
31. “Kifo hakitakuwapo tena.”—Ufu. 21:3, 4; Isa. 25:8.
DINI
-
32. Si dini zote zinazompendeza Mungu.—Yer. 7:11; Mt. 7:13, 14, 21-23.
-
33. Mungu anachukia unafiki.—Isa. 29:13; Mika 3:11; Marko 7:6-8.
-
34. Upendo wa kweli hutambulisha dini ya kweli.—Mika 4:3; Yoh. 13:34, 35.