Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Mtu Aliyeubadili Ulimwengu

Mtu Aliyeubadili Ulimwengu

Mtu Aliyeubadili Ulimwengu

Mabilioni ya watu wameishi duniani. Wengi wao wamesahaulika. Hata hivyo, wachache wamebadili hali ya watu ulimwenguni na yaelekea hata maisha yako ya kila siku.

UNAAMKA asubuhi ili kujitayarisha kwenda kazini. Unawasha taa kabla ya kuanza kujitayarisha. Unachukua kitabu au gazeti la kusoma unaposafiri kwa basi kuelekea kazini. Unakumbuka kutumia dawa ambayo umepewa na daktari kwa sababu umeambukizwa ugonjwa fulani. Ni mapema asubuhi, lakini tayari umenufaika na kazi ya watu wachache maarufu.

Michael Faraday Mwanafizikia huyu Mwingereza alizaliwa mwaka wa 1791. Alibuni mota ya umeme na chombo cha kuzalisha umeme kinachoitwa dainamo. Mambo aliyovumbua na vitu alivyobuni vimewawezesha wanadamu kutumia umeme kwa njia nyingi.

Ts’ai Lun Alikuwa afisa wa maliki wa China aliyebuni njia ya kutengeneza karatasi yapata mwaka wa 105 W.K. Ubuni huo ulisaidia kutengeneza karatasi kwa wingi sana.

Johannes Gutenberg Mnamo mwaka wa 1450, mvumbuzi huyu Mjerumani alibuni mashine ya kwanza ya kuchapia yenye herufi za kupangwa. Kwa sababu ya mashine hii, gharama za kuchapa zilipungua na hivyo watu wengi waliweza kusoma habari nyingi kuhusu mambo mbalimbali.

Alexander Fleming Mtafiti huyu Mskoti alivumbua dawa ya kuua viini aliyoiita penisilini mnamo mwaka wa 1928. Dawa za kutibu magonjwa yanayosababishwa na viini, au bakteria, zinatumiwa sana leo.

Bila shaka, uvumbuzi na vitu vilivyobuniwa na watu wachache vimewanufaisha watu wengi sana au kuboresha afya zao.

Hata hivyo, mtu mmoja amewapita wote. Umaarufu wake hautokani na uvumbuzi fulani wa kisayansi au kitiba. Badala yake, mtu huyu aliyelelewa na wazazi maskini na aliyekufa karibu miaka 2,000 iliyopita, alihubiri ujumbe wenye nguvu wa tumaini na faraja. Tunapofikiria kiwango ambacho ujumbe wake umewanufaisha watu duniani kote, wengi wanakubali kwamba yeye ndiye aliyeubadili ulimwengu kikweli.

Mtu huyu ni Yesu Kristo. Alihubiri ujumbe gani? Na wewe unaweza kunufaika na ujumbe wake jinsi gani?