Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

HABARI KUU | KWA NINI WATU WAZURI HUPATWA NA MAMBO MABAYA?

Mambo Mabaya Yameenea Kote!

Mambo Mabaya Yameenea Kote!

Smita, * mwanamke mwenye umri wa miaka 35 aliyeishi huko Dhaka, Bangladesh, aliwapenda na kuwajali sana watu. Alijulikana kuwa mke mwenye bidii na furaha aliyetaka kuwasaidia watu wajue mambo aliyokuwa amejifunza kumhusu Mungu. Familia na rafiki zake walishtuka sana Smita alipopatwa ghafula na ugonjwa na kufa baada ya siku chache tu!

James na mkewe, wenzi wa ndoa waliokuwa na umri wa miaka 30 hivi, walikuwa na sifa kama za Smita. Pindi fulani, walienda kutembelea rafiki zao huko pwani ya magharibi ya Marekani. Hawakurudi tena nyumbani kwao, New York. Wakiwa safarini, walipata aksidenti mbaya ya barabarani wakafa, na hivyo kuacha pengo kubwa katika maisha ya wapendwa wao na wafanyakazi wenzao.

Hatuhitaji kutazama mbali ili kuona jinsi uovu na mateso yalivyoenea ulimwenguni leo. Vita huua raia na vilevile wanajeshi. Watu wasio na hatia huteseka kwa sababu ya jeuri na uhalifu. Aksidenti mbaya na magonjwa yenye kulemaza humpata mtu yeyote bila kujali umri au hali yake maishani. Misiba ya asili hutokea popote bila kuchagua jamii hususa. Ubaguzi na ukosefu wa haki umeenea sana. Labda wewe binafsi umekumbwa na hali hizo.

Ni jambo la kawaida kujiuliza maswali yafuatayo:

  • Kwa nini watu wazuri hupatwa na mambo mabaya?

  • Je, Mungu ndiye anayesababisha mambo hayo?

  • Je, misiba hutokea yenyewe, au inasababishwa na wanadamu?

  • Je, mateso yanasababishwa na Karma, yaani, matokeo ya matendo ya mtu katika uhai uliotangulia?

  • Ikiwa kuna Mungu mweza-yote, kwa nini hawalindi watu wazuri wasipatwe na mabaya?

  • Je, kuna wakati ambapo hakutakuwa tena na uovu na kuteseka?

Ili kujibu maswali hayo, tunahitaji kupata majibu ya maswali haya mawili ya msingi: Kwa nini mambo mabaya huwapata watu wote, na Mungu atafanya nini?

^ fu. 3 Majina yamebadilishwa.