Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Thai Liang Lim/E+ via Getty Images

ENDELEA KUKESHA!

Je, Mitandao ya Kijamii Inamdhuru Mtoto Wako?​—⁠Biblia Inaweza Kuwasaidiaje Wazazi?

Je, Mitandao ya Kijamii Inamdhuru Mtoto Wako?​—⁠Biblia Inaweza Kuwasaidiaje Wazazi?

 “Tatizo la afya ya akili limekuwa kubwa sana miongoni mwa vijana—na imegunduliwa kwamba mojawapo ya visababishi vikubwa ni mitandao ya kijamii.”​—Dakt. Vivek Murthy, U.S. surgeon general, New York Times, Juni 17, 2024.

 Wazazi wanaweza kuwalindaje watoto wao kutokana na hatari za mitandao ya kijamii? Biblia inatupatia ushauri unaofaa.

Wazazi wanaweza kufanya nini?

 Fikiria kanuni hizi za Biblia.

 “Mwerevu hutafakari kila hatua.”​—Methali 14:15.

 Kwa kuwa mitandao ya kijamii inaweza kumdhuru mtoto wako, usihisi kwamba ni lazima umruhusu atumie mitandao hiyo. Kabla ya kumruhusu, hakikisha kwamba yeye ni mkomavu vya kutosha kufuata sheria kuhusu muda anaoruhusiwa kutumia mitandao hiyo, kudumisha urafiki unaofaa, na kuepuka habari zisizofaa.

 ‘Tumia vizuri kabisa wakati wako.’​—Waefeso 5:16.

 Ukimruhusu mtoto wako kutumia mitandao ya kijamii, weka sheria zinazoonyesha jinsi anavyopaswa kuitumia, na ueleze jinsi sheria hizo zitakavyomsaidia kuwa salama. Uwe macho kuona ikiwa tabia ya mtoto wako inabadilika kwa njia yoyote, kwa kuwa hilo litakusaidia kuamua ikiwa unapaswa kudhibiti matumizi yake ya mitandao hiyo.

  •   Tumia video ya vibonzo kwenye ubao yenye kichwa Tumia Mitandao ya Kijamii kwa Hekima ili kumsaidia mtoto wako kuelewa kwa nini tunahitaji kudhibiti jinsi tunavyotumia mitandao hiyo.

Jifunze mengi zaidi

 Biblia inasema kwamba tunaishi katika “nyakati za hatari zilizo ngumu kushughulika nazo.” (2 Timotheo 3:1-5) Wakati uleule inatupatia ushauri unaofaa unaweza kutusaidia kukabiliana na nyakati hizi. Orodha ya zaidi ya makala 20 zinazotegemea Biblia inapatikana katika makala hii kuhusu afya ya akili ya vijana. Makala zote hizo zina habari kwa ajili ya wazazi na watoto wao.