Hamia kwenye habari

Baadhi ya ndugu 65 walioachiliwa mapema kutoka gerezani baada ya uamuzi wa Mahakama Kuu ya Korea Kusini kutangaza kwamba msimamo wao unaotegemea dhamiri si tendo la uhalifu.

MACHI 7, 2019
KOREA KUSINI

Mashahidi Wote Waliofungwa kwa Kukataa Kujiunga na Jeshi kwa Sababu ya Dhamiri Nchini Korea Kusini Wameachiliwa

Mashahidi Wote Waliofungwa kwa Kukataa Kujiunga na Jeshi kwa Sababu ya Dhamiri Nchini Korea Kusini Wameachiliwa

Februari 28, 2019, Shahidi wa mwisho nchini Korea Kusini aliyekuwa gerezani kwa sababu ya msimamo wa kutojiunga na jeshi ameachiliwa. Ndugu wote walioachiliwa wameshukuru sana kupata uhuru na fursa waliyokuwa nayo ya kuthibitisha ushikamanifu wao kwa Yehova Mungu.

Jumla ya ndugu 65 wameachiliwa tangu uamuzi wa kihistoria wa Mahakama Kuu uliotolewa Novemba 1, 2018, ambao ulitangaza kwamba kukataa kujiunga na jeshi kwa sababu ya dhamiri si tendo la uhalifu. Uamuzi huo umekomesha desturi ya miaka 65 ya kuwafunga gerezani wale wanaokataa kujiunga na jeshi kwa sababu ya dhamiri.

Imani na utimilifu wa ndugu zetu nchini Korea unatuchochea ‘kuonyesha uhodari mwingi’ katika utumishi wetu mshikamanifu kwa Mfalme wetu na Ufalme wake. (Wafilipi 1:14) Tunasali kwa ajili ya ndugu zetu ambao bado wamefungwa nchini Eritrea, Urusi, Singapore, na Turkmenistan.—Waebrania 10:34.