Hamia kwenye habari

Kushoto hadi kulia: Ndugu Vladimir Bukin, Mikhail Burkov, Valeriy Slashchev, na Sergey Yuferov

JANUARI 26, 2022 | HABARI ZA KARIBUNI: JUNI 27, 2023
URUSI

HABARI ZA KARIBUNI—NDUGU WAMEFUNGWA | Kuwasaidia Wengine na Kumtumaini Yehova Kunawategemeza Ndugu Huko Tynda

HABARI ZA KARIBUNI—NDUGU WAMEFUNGWA | Kuwasaidia Wengine na Kumtumaini Yehova Kunawategemeza Ndugu Huko Tynda

Juni 27, 2023, Mahakama ya Wilaya ya Tyndinskiy iliyo katika Eneo la Amur iliwahukumu Ndugu Vladimir Bukin, Ndugu Mikhail Burkov, Ndugu Valeriy Slashchev, na Ndugu Sergey Yuferov kifungo cha gerezani. Mikhail alihukumiwa kifungo cha miaka sita na miezi mwili gerezani. Vladimir, Valeriy, na Sergey walihukumiwa kifungo cha miaka sita na miezi minne gerezani. Ndugu wote wanne walipelekwa gerezani mara moja.

Desemba 27, 2022, Mahakama ya Eneo la Amur ilipindua uamuzi wa kuwahukumu Vladimir, Mikhail, Valeriy, na Sergey na ikaamuru kesi yao ianze kusikilizwa upya. Ndugu hao waliachiliwa kutoka gerezani na wanasubiri kesi yao isikilizwe upya. Hata hivyo, wamezuiwa kuondoka katika eneo hilo.

Oktoba 25, 2022, Mahakama ya Wilaya ya Tyndinskiy katika Eneo la Amur iliwahukumu Vladimir, Mikhail, Valeriy, na Sergey. Vladimir, Valeriy, na Sergey walipewa kifungo cha miaka sita na nusu gerezani, kila mmoja. Mikhail alipewa kifungo cha miaka sita na miezi miwili. Ndugu wote wanne walipelekwa gerezani mara tu baada ya hukumu hiyo kutolewa mahakamani.

Mfuatano wa Matukio

  1. Novemba 17, 2019

    Maofisa wa usalama walifanya upekuzi katika nyumba za familia nane za Mashahidi wa Yehova katika eneo hilo, kutia ndani nyumba za ndugu hao wanne

  2. Novemba 18, 2019

    Wapelelezi waliwashtaki ndugu wote wanne kuwa wenye msimamo mkali. Waliwekwa chini ya masharti yaliyowazuia kuondoka eneo hilo

  3. Julai 26, 2021

    Kesi ya uhalifu ilianza

Maelezo Mafupi Kuwahusu

Tuna uhakika kwamba Yehova ataendelea ‘kuwatendea kwa upendo mshikamanifu’ ndugu zetu wapendwa na watumishi wake wote waaminifu.​—Mwanzo 39:21.