MEI 23, 2024
URUSI
“Yehova Atakuwa Pamoja Nami”
Mahakama ya Wilaya ya Urupskiy iliyo katika Jamhuri ya Karachayevo-Circassian itatangaza uamuzi wake hivi karibuni katika kesi inayomhusu Ndugu Aleksey Pasynkov. Mwendesha mashtaka bado hajatoa ombi la hukumu anayopendekeza.
Maelezo Mafupi Kumhusu
Tunafurahi sana kujua kwamba hata ingawa tunakabili majaribu mbalimbali, sikuzote tunaweza kupata kimbilio na shangwe katika Yehova.—Zaburi 5:11.
Mfuatano wa Matukio
Novemba 23, 2021
Wenye mamlaka walimkamata Aleksey kwenye eneo lake la kazi, kisha wakafanya msako nyumbani kwake
Desemba 8, 2022
Kesi ya uhalifu ilifunguliwa
Machi 3, 2023
Nyumba ilifanyiwa msako kwa mara ya pili. Aleksey na Yuliya wakahojiwa
Machi 31, 2023
Nyumba ya mama ya Aleksey na kaka zake zilifanyiwa msako
Oktoba 4, 2023
Aliwekewa vizuizi vya kusafiri
Desemba 14, 2023
Kesi ya uhalifu ilianza