Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

TOVUTI YA JW.ORG

Maswali Yanayoulizwa Mara Nyingi​—JW.ORG

Maswali Yanayoulizwa Mara Nyingi​—JW.ORG

Visakuzi vingi vya kisasa vinategemezwa. Visakuzi vya zamani ambavyo havisasishwi kwa ukawaida na watengenezaji wake ili kuwa salama, huenda visifanye kazi. Utafaidika sana ukitumia kisakuzi cha kisasa zaidi.

Visakuzi vifuatavyo havitegemezwi:

  • Internet Explorer toleo la 8 na kabla. Ikiwa unatumia kompyuta iliyo na mfumo wa uendeshaji wa mapema zaidi ambao hautegemezi matoleo ya awali ya Internet Explorer, tafadhali tumia kisakuzi kingine.

  • Opera Mini

Utegemezo kwa vifaa vya mkononi vyenye mifumo ya uendeshaji ifuatayo unapatikana:

  • Android 4.2 au wa karibuni zaidi

  • iOS 9.0 au wa karibuni zaidi (utegemezo wa kiasi kwa vifaa vyenye mifumo ya uendeshaji ya zamani)

 

Kuna njia kadhaa za kufanya hivyo, kutia ndani zifuatazo:

  • Pakua programu ya JW Broadcasting, inayopatikana kwa ajili ya Amazon Fire TV, Apple TV (toleo la 4), na king’amuzi cha Roku.

  • Ikiwa una televisheni yenye uwezo wa kutumia intaneti (Smart TV), unaweza kufungua tovuti ya jw.org na kucheza video. Hata hivyo, si kila televisheni ya aina hiyo itakayofaa. Hivyo, video hazichezi katika kila televisheni za aina hiyo.

    Unaweza pia kutumia kompyuta au simu ya mkononi kutazama video katika televisheni yako. Njia hizo zinafanya kazi ikiwa utatazama video kupitia tovuti ya jw.org na ili kucheza video ulizopakua katika kifaa chako.

  • Ikiwa una kompyuta ya Apple au simu na kifaa cha Apple TV, unaweza kutumia AirPlay kutazama video katika televisheni yako. Tembelea tovuti ya Apple sehemu ya msaada ili upate taarifa zaidi.

  • Ikiwa unatumia kifaa cha Google Chromecast, unaweza kutazama video kwa kuzirusha katika televisheni yako kutoka kwenye kisakuzi cha Chrome. Tembelea tovuti ya Google sehemu ya msaada ili upate taarifa zaidi.

  • Unaweza kuunganisha kompyuta, tablet, au simu katika televisheni yako kwa kutumia waya wa HDMI, DVI, VGA, au S-Video. Soma maelekezo ya kitabu cha mwongozo cha kompyuta au simu na televisheni yako ili ufanye uchaguzi utakaokufaa.