Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

INDONESIA

Biashara ya Viungo

Biashara ya Viungo

KATIKA karne ya 16, biashara ya viungo ilichangia sana ukuzi wa uchumi wa ulimwengu kama tu ilivyo biashara ya mafuta ghafi leo. Viungo kama vile kungumanga, na karafuu vilitoka kisiwa maarufu cha Spice Islands (sasa ni mikoa ya Maluku na Maluku Kaskazini nchini Indonesia), vilipata soko kubwa sana Ulaya.

Wavumbuzi kama vile Christopher Columbus, Vasco da Gama, Ferdinand Magellan, Samuel de Champlain, na Henry Hudson walitembelea kisiwa cha Spice Islands. Jitihada za kutafuta viungo kutoka Indonesia ziliwafanya watu waifahamu vizuri zaidi sayari yetu.