Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

INDONESIA

Niliokoka Machafuko ya Ukomunisti

Ronald Jacka

Niliokoka Machafuko ya Ukomunisti
  • ALIZALIWA 1928

  • ALIBATIZWA 1941

  • HISTORIA FUPI Alitumikia akiwa mtumishi wa tawi nchini Indonesia kwa zaidi ya miaka 25.

ASUBUHI ya Oktoba 1, 1965, vikosi vya jeshi vilivyohusianishwa na chama cha Indonesian Communist Party (PKI) viliwaua majenerali sita katika jaribio la kufanya mapinduzi. Serikali ilijibu mashambulizi hayo kikatili na kwa haraka. Mauaji hayo yanaelezwa kuwa “mauaji makubwa ya kijeuri” ya kitaifa, ambapo watu 500,000 hivi walioshukiwa kuwa wakomunisti waliuawa.

Majuma kadhaa baada ya mapinduzi hayo kushindwa, kamanda mkuu wa jeshi aliniambia kwamba jina langu lilikuwa la kwanza katika orodha ya viongozi wa dini ambao wakomunisti walikuwa wamepanga kuwaua. Pia, alijitolea kwenda kunionyesha kaburi ambalo lilikuwa limeandaliwa kwa ajili ya kunizika, hata hivyo, nilikataa kwa upole. Nisingependa kumuunga mkono katika mazingira hayo ya kisiasa, na kuharibu msimamo wangu wa Kikristo wa kutounga mkono upande wowote