FEBRUARI 23, 2021
JAPANI
Tetemeko la Ardhi Lapiga Japani Kaskazini-Mashariki
Mahali
Kaskazini-mashariki mwa Japani, hasa majimbo ya Fukushima na Miyagi
Janga
Februari 13, 2021, tetemeko la ardhi lenye kipimo cha 7.3 lilisababisha ukosefu wa umeme na maji katika maeneo fulani. Uharibifu mkubwa ulitokea katika maeneo yaleyale yaliyokuwa yamekumbwa na tetemeko kubwa lenye kipimo cha 9.0 mnamo 2011
Athari ambazo ndugu na dada zetu wamepata
Wahubiri 11 walijeruhiwa
Ndugu wengi walikosa umeme na maji kwa muda fulani
Uharibifu wa mali
Majumba 10 ya Ufalme yalipata uharibifu mdogo
Nyumba 205 zilipata uharibifu mdogo
Nyumba 13 zilipata uharibifu mkubwa
Jitihada za kutoa msaada
Waangalizi wa mzunguko na wazee wa makutaniko katika maeneo yaliyoathiriwa wanawaandalia wahubiri msaada wa kiroho kupatana na miongozo ya kujilinda dhidi ya ugonjwa wa COVID-19
Wawakilishi wa Idara ya Usanifu-Majengo na Ujenzi pamoja na wajitoleaji wa idara hiyo wanachunguza kiwango cha uharibifu katika kila Jumba la Ufalme na nyumba za akina ndugu
Tunasali kwamba Yehova aendelee kuwaimarisha walioathiriwa na tetemeko hilo la ardhi.—Wafilipi 4:13.