JULAI 20, 2017
JAPANI
Mvua Kubwa Imesababisha Mafuriko Kyushu, Japani
Baada ya Kimbunga Nanmadol kupiga maeneo ya kusini ya Japani, kulikuwa na mvua nyingi sana zilipiga eneo la Kyushu, kisiwa cha tatu kwa ukubwa, Jumatano, Julai 5, 2017, ambazo zilisababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi na kuwafanya wenye mamlaka watoe agizo la kuwahamisha watu zaidi ya 430,000 walioishi katika maeneo yaliyoathiriwa. Mvua ilinyesha kwa kipindi cha saa 12 na ilikuwa na kiwango cha ujazo wa milimita 508 hivi. Ripoti fulani zinaonyesha kwamba watu 34 hivi walikufa kutokana na mafuriko. Fukuoka ni mojawapo ya maeneo yaliyoathiriwa sana katika eneo la kaskazini la Kyushu.
Hakuna Mashahidi wa Yehova walioripotiwa kujeruhiwa au kuuawa, lakini nyumba kadhaa ziliharibiwa na mafuriko. Makutaniko ya Mashahidi wa Yehova yanatoa msaada wa kutunza mahitaji ya waabudu wenzao.
Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:
David A. Semonian, Ofisi ya Habari za Umma, simu +1-845-524-3000
Japani: Ichiki Matsunaga, simu +81-46-233-0005